MAREKANI

Joe Biden kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa Septemba 21

Joe Biden, ambaye amekosolewa baada ya kuyatoa majeshi yake nchini Afghanistan jambo ambalo pia lilipokelewa kwa shingo upande na baadhi ya washirika wa Marekani, kwa hivyo atazindua mfululizo wa mikutano kadhaa ya kidiplomasia.
Joe Biden, ambaye amekosolewa baada ya kuyatoa majeshi yake nchini Afghanistan jambo ambalo pia lilipokelewa kwa shingo upande na baadhi ya washirika wa Marekani, kwa hivyo atazindua mfululizo wa mikutano kadhaa ya kidiplomasia. REUTERS - KEVIN LAMARQUE

Rais wa Marekani Joe Biden anatarajia kuhutubia Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa huko New York Septemba 21, Ikulu ya White House imesema katika taarifa.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano huo, ambao ulifanyika hasa kupitia video mwaka jana kwa sababu ya janga Covid-19, wakati huu utafanyika kwa muundo wa mseto ambapo watashiriki moja kwa moja viongozi mbalimbali wa dunia kwa sharti la kutokaribiana. Wakuu wa nchi na serikali mia moja wametangaza utayari wao wa kwenda New York, kulingana na orodha ya awali ya washiriki ambayo shirika la habari la AFPO limepata kopi Jumanne hii Septemba 14.

Masharti makali ya usafi kutokana na janga Covid-19

Masharti makali yametangazwa, na idadi ya watu kwa kila ujumbe imepunguzwa hadi watu 7. Kuwa umeepokea chanjo  dhidi ya Covid-19 na kipimo kinachoonyesha kuwa hauna maambukizi ya virusi vya gonjwa hilo.

Joe Biden, ambaye amekosolewa baada ya kuyatoa majeshi yake nchini Afghanistan jambo ambalo pia lilipokelewa kwa shingo upande na baadhi ya washirika wa Marekani, kwa hivyo atazindua mfululizo wa mikutano kadhaa ya kidiplomasia.

Septemba 24, Joe Biden atapokea Mawaziri Wakuu wa Australia, India na Japan katika Ikulu ya White House.

Kwa hivyo anakusudia kufufua "mazungumzo ya usalama ya pande nne", muundo ambao Washington inataka kuunda dhidi ya jitihada za China katika ukanda wa Indo-Pacific.

Baadaye, mwishoni mwa mwezi wa Oktoba na mwanzoni mwa mwezi wa Novemba, itafuata mkutano wa G20 na mkutano mkuu wa tabia nchi wa COP26. Na mwishowe, mwanzoni mwa mwezi wa Desemba, "mkutano wa kilele kuhusu demokrasia" ambao rais wa Marekani anataka kuandaa katika muundo halisi, na ambao orodha ya washiriki bado haijajulikana.