MAREKANI-SIASA

Kura ya maoni California: Gavana kutoka chama cha Democratic ashinda

Gavana wa Gavin Newsom akizungumza huko San Francisco Septemba 14, 2021.
Gavana wa Gavin Newsom akizungumza huko San Francisco Septemba 14, 2021. Getty Images via AFP - JUSTIN SULLIVAN

Gavin Newsom anaendelea kushikilia nafasi yake ya Gavana wa California, jimbo lenye watu wengi na tajiri zaidi nchini Marekani. Chini ya saa moja baada ya kufungwa kwa vituo vya kupigia kura Jumanne, Septemba 14, kura ya "hapana" ilishinda kwa zaidi ya 66% dhidi ya 60% ya kura ambazo tayari zimehesabiwa, kulingana na vituo vya habari vya CNN na NBC.

Matangazo ya kibiashara

Chama cha Democratic kilitarajia kushinda kwa kura nyingi kabisa ili kuepuka kutimuliwa kwa Gavana Gavin Newsom. Ni ushindi kwa Gavin Newsom, lakini pia kwa rais Joe Biden, ambaye alikuja kumuunga mkono gavana huyo usiku wa kuamkia siku hiyo kufanyika kwa kura ya maoni.

Hakukuwa na mashaka hata kidogo. Kuanzia uchaguzi wa kwanza, ilikuwa wazi kabisa kwamba California ingelitawaliwa na mjumbe kutoka chama cha Democratic, kama kawaida. Huu ni ushindi wa Gavana Newsom, ambaye sera yake kali dhidi ya Covid-19 hapo awali ilikosolewa kabla ya kuonekana kuwa yenye ufanisi wakati wa ilipoongezeka idadi ya visa vya maambukizi ya aina mpya ya Corona, Delta.

Gavin Newsom alikuwa akipambana dhidi ya Larry Elder kutoka chama cha Republican. Mgombea huyo mkuu wa chama cha Republican anaunga mkono hoja za Donald Trump, hasa kuhusu udanganyifu katika uchaguzi wa urais uliyopita. Na kwa upande wa Gavin Newsom, anapinga hoja hiyo.