MEXICO-HAKI

Mexico: Mke wa "El Mancho", kiongozi mwenye nguvu wa kundi la Jalisco, akamatwa

Mamlaka ya Mexico ilitangaza Jumanne (Novemba 16) kukamatwa kwa mke wa Nemesio Oseguera, anayejulikana kama "El Mencho", kiongozi wa genge la Jalisco New Generation, mlanguzi wa dawa za kulevya mwenye nguvu zaidi nchini. Kukamatwa huku ni "pigo kwa muundo wa kifedha wa uhalifu uliopangwa", kulingana na Wizara ya Ulinzi.

Wanajeshi wa Mexico wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Jalisco Nueva Generacion.
Wanajeshi wa Mexico wakati wa operesheni dhidi ya kundi la Jalisco Nueva Generacion. AFP PHOTO/Hector Guerrero
Matangazo ya kibiashara

Rosalinda González Valencia alikuwa tayari amekamatwa Mei 2018 kwa utakatishaji fedha, kisha kuachiliwa baada ya kulipa dhamana yake. Leo, anashutumiwa kuwa na jukumu la "operesheni haramu za kifedha za kikundi cha wahalifu kilichopangwa", ikimaanisha chochote kinachohusiana na ununuzi, ufichaji na uhamishaji wa pesa kwenye katika ardhi hiyo kwa niaba ya shirika hilo.

Mumewe, Nemesio Oseguera, kwa jina la utani "El Mencho", ni afisa wa zamani wa polisi ambaye alikua kiongozi wa kundi la Jalisco New Generation. Ni mpinzani mkuu wa kundi la Sinaloa, lililokuwa likiongozwa na Joaquín "El Chapo" Guzmán.

Kukamatwa huku kunakuja siku mbili kabla ya mkutano wa kwanza wa kilele wa Mexico-Marekani-Canada katika miaka mitano, ambao unapanga kushughulikia maswala ya usalama na ulanguzi wa dawa za kulevya.