THAILAND

Yingluck Shinawatra ateuliwa kuwania uwaziri mkuu wa Thailand

© Reuters

Kwa mara ya kwanza katika historia ya siasa za Thailand ,mgombea mwanamke ameteuliwa kuwania nafasi ya uwaziri mkuu wa nchi hiyo kupitia chama kikuu cha upinzani.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuteuliwa kwa bi. Yingluck Shinawatra inaonekana kufunikwa zaidi na ukweli kuwa mgombea huyo ni dada wa aliyekuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Thaksin Shinawatra.

Bi. Yongluck ambaye hana uzoefu wa masuala ya siasa atakuwa na kibarua kigumu cha kuithibitishia dunia kuwa anastahili nafasi hiyo na sik kibaraka wa kaka yake kama ambavyo inatafsiriwa na wengi.

Bi. Yingluck mwenye umri wa miaka arobaini na mitatu na ambaye taaluma yake ni bisahara ni mtu wa karibu wa Thaksin baada ya mke wake.

Uteuzi huo pia umeonesha namna Shinawatra alivyo na ushawishi katika siasa za Thailand hata wakati huu ambapo anaishi uhamishoni.

Thaksin anatuhumiwa kuchochea ghasia wakati wa maandamano makubwa ya wafuasi wake wa mashati mekundu yaliyofanyika mwaka jana na kusababisha watu kadhaa kupoteza maisha.Thaksin pia anatuhumiwa kushiriki katika ugaidi.