Syria

Upinzani nchini Syria watoa mwito wa mgomo na maandamano kwa mara nyingine jumatano hii.

Mji wa Banias kati y amiji inayo shuhudia maandamano
Mji wa Banias kati y amiji inayo shuhudia maandamano REUTERS

Wakati vuguvugu la maandamano nchini Syria likiingia katika mwezi wake wa tatu, upinzani watoa mwito kwa raia wa nchi hiyo kukusanyika katika maeneo mbalilbali jumatano hii Mei 18 na kuandamana. Mbali na maandamano, hakuna shule, hakuna biashara, usafiri na mengine. Maandamano hayo yalianza Machi 15 katika miji mbalimbali ya nchi hiyo, ispokuwa mji mkuu Damas na mji wa pili wa nchi hiyo wa Alep.

Matangazo ya kibiashara

Deraa imekuwa makao makuu ya vuguvugu la maandamano ya Syria. Miji mingine mingi inaitikia wito wa mgomo na maandamano yanayo itishwa na upinzani.
Salim Monaim ni mpinzani wa Syria, pia ni mwanachama wa baraza la kitaifa la mkataba wa Damas, anaetaka mabadiliko ya kidemokrasia nchini Syria. Akiwa wakati huu mjini Paris amefahamisha mbinu alizotumia rais wa nchi hiyo Bashar al Assad ili kuidhibiti miji ya Damas na Alp.” Utawala uliwatuma polisi wengi wakivalia ngua za kawaida katika miji ya Damas na Alep ili kuwazuia wartu wasitoki. Kwa mfano Alep kuna polisi elfu 30. labda Damas wako wengi zaidi na huenda ni mara mbili ya hao”

Salim Monaim amesema wakaazi wa vitongoji vya mji wa Damas Mouadamiya na Quatan, navyo pia vilijiunga na vuguvugu hilo la maandamano, lakini hata hivyo ili mji mkuu kabisa uingia katika vuguvugu hilo inabidi wanajeshi na polisi wajiunge na waandamanji.

Siku ambayo wananchi wa miji ya Damas na Alep watakuwa na uwezo wa kujiunga na vuguvugu hilo la maandamano, ndio siku utawala wa Syria utakuwa karibu ya kuondoka, athibitisha hayo Salim Monaim.

Kaburi la pamoja la Deera

shirika la kimataifa la haki za binadamu nchini Syria limesema kaburi la pamoja la pili limegumduliwa jumanne Mei 17, karibu na eneo kulikogunduliwa kaburi lingine kama hilo siku za nyuma kusini mwa mji wa Deera. Kaburi hilo la pamoja lilikuwemo miili 24, lingine miili 7. Serikali ya Syria kupitia waziri wake wa mambo ya ndani imekanusha habari hii na kusema kuwa miili 5 pekee ndio iliogunduliwa.