Pakistani-Taliban

Watu 8 wauawa katika shambulio la kujitoa muhanga nchini Pakistan

Shambulio la Bomu lililo wauwa watu kadhaa nchini Pakistan
Shambulio la Bomu lililo wauwa watu kadhaa nchini Pakistan REUTERS/Fayaz Aziz

Shambulizi la kujitoa mhanga lililotekelezwa katika Kituo cha Polisi nchini Pakistani na wanamgambo wa Kundi la Taliban limesababisha vifo vya watu wanane ukiwa ni muendelezo wa kulipiza kisasi cha kifo cha Kiongozi wa Al Qaeda Osama Bin Laden.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo limetekelezwa kwa kutumia lori likitokea Kaskazini Magharibi mwa Jiji la Peshawar ikiwa siku moja baada ya Msafara wa Marekani kufanya mashambulizi kuwalenga Wanamgambo wa Taliban.

Kundi la Wanamgambo wa Taliban limethibitisha kushiriki kwenye kupanga na hatimaye kutekeleza shambulizi hilo na kusema hili ni la nne katika muendelezo wao wa kulipiza kisasi cha kifo cha Osama kilichotokea tarehe mbili ya mwezi Mei.