China, Korea

Kiongozi wa Korea Kaskazini azuru nchini China

Rais wa China Hu Jintao na rais wa Korea Kim Jing
Rais wa China Hu Jintao na rais wa Korea Kim Jing 照片来源:路透社

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Il ambaye amezuru China amemwambia Rais wa nchi hiyo Hu Jintao ya kwamba nchi yake inahitaji uwepo wa mazingira yenye kuvutia ili iweze kukua kiuchumi.

Matangazo ya kibiashara

Kim amesema nchi yake imekuwa ikifanya kila linalowezekana katika kuhakikisha uchumi wake unastawi kwa kiwango cha hali ya juu lakini hilo haliwezi kufikiwa iwapo mazingira yatakuwa kikwazo.

Rais Kim ambaye amefanya ziara ya kushtukiza nchini China amesema nchi yake ipo tayari kuruhusu kujadiliwa kwa suala la nyuklia ambalo limekuwa likishirikisha pande sita ambazo ni pamoja na Korea Kusini, Marekani, Japan na Urusi.