Pakistani-Taliban

Watu 12 wauawa kwa mlipuko wa bomu la kutegwa ardhini nchini Pakistsani

Bomu lililotengwa karibu na mahakama moja iliyopo Kaskazini Magharibi mwa Mji wa Hangu nchini Pakistani limesababisha vifo vya watu kumi na mbili huku wengine kumi na moja wakijeruhiwa.

Eneo lililo shuhudia mlipuko wa bomu la kutegwa
Eneo lililo shuhudia mlipuko wa bomu la kutegwa REUTERS/M. Abdullah
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Polisi wa Wilaya hiyo Abdul Rashid Khan amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza bomu hilo lilitegwa kwenye gari ambalo lilienda kuegeshwa pembeni ya jengo la mahakama.

Tayari Kundi la Wanamgambo wa Talibani wamejinadi kutekeleza shambulizi hilo wakisema huu ni muendelezo wa mashambulizi yao ya kuliza kisasi cha Kifo cha Kiongozi wa Al Qaeda Duniani Osama Bin Laden.