Syria

Majeshi ya Syria yandelea na harakati ya kuwasambaratisha waandamanaji

Telegrame.com

Majeshi ya Serikali ya Syria yameendelea kutumia nguvu kuwasambaratisha maelfu ya wananchi waliojitokeza kwenye maandamano ya kushinikiza kuondoka madarakani kwa serikali ya Rais Bashar Al Assad.

Matangazo ya kibiashara

Ni siku Ijumaa ambayo imeshuhudia sarat Ijumaa ikikamilika kwa usalama nchini Syria kisha waumini wakiambatana na wananchi wengine wakivamia mitaa mbalimbali kushinikiza kuondoka madarakani kwa serikali ya Rais Assad.

Shinikizo hilo linakumbana na kikwazo ambacho ni majeshi ya serikali ambayo yakiwa na zana za kivita wanawafyatulia risasi waandamanaji na kusababisha vifo vya watu sita ambao walijitokeza.

Wanaharakati wameendelea kushirikiana na wananchi katika kuhakikisha wanapaza sauti kutaka mabadiliko yafanyike nchini Syria haraka iwezekanavyo wakidai wamechoshwa na Utawala wa Rais Assad.

Tayari Ufaransa kupitia Rais wake Nicolas Sarkozy imeendelea kulaani ukiukwaji mkubwa wa haki unaofanywa na serikali ya Rais Assad na kutaka mabadiliko yafanyike sasa huku wakiomba suala la kupitishwa kwa Azimio la Umoja wa Mataifa liungwe mkono.

Machafuko haya yameendelea kuiathiri nchini jirani ya Uturuki ambayo imeendelea kuwa kimbilio la wakimbizi kutoka Syria wakiomba hifadhi kutokana na mapigano kuendelea kuchacha nchini mwao.