Iraq

Mlipuko wa bomu wajeruhi wa 7 mjini Bagdad

Gari la msafara wa ubalozi wa ufaransa likilupuka kwa moto kusini mwa Bagdad
Gari la msafara wa ubalozi wa ufaransa likilupuka kwa moto kusini mwa Bagdad Metrofrance

Watu 7 raia wa Iraq wamejeruhiwa na mlipuko wa bomu uliolenga msafara wa Balozi wa Ufaransa mapema asubuhi ya Jumatatu Juni 30 kusini mwa Bagdad, imethibitisha hivyo duru kutoka wizara ya mambo ya kigeni.

Matangazo ya kibiashara

Walinzi 4 wa Ubalozi w ufaransa raia wa Irak na wapitanjia 3 wamejeruhiwa katika mlipuko wa bomu lilolipuka katika msafara wa kidiplomasia katika kata ya Masbah

Gari moja la ubalozi wa ufaransa lililo haribiwa na bomu hilo limebakia katika eneo hilo la tukio, amethibitisha muandishi wa habari wa AFP alieshuhudia na kusem akuwa tukio hilo limetokea sio mbali na makaazi ya Balozi wa Ufaransa.

Muakilishi wa Ubalizi wa ufaransa mjini Bagdad amekiri kutoke kwa tukio hilo lakini hakuwa tayari kuzungumzia hasara zilizo tokana na shambulizi hilo.