Brazili

Polisi ya Brazili yaendesha msako kuhakikisha usalama unadhibitiwa miaka 3 kabla ya kombe la dunia

Helikopta ya brezil
Helikopta ya brezil REUTERS/Sergio Moraes

Mamia ya polisi na askari nchini Brazil, wakisaidiwa na helikopta na magari ya kijeshi yamefanya msako mkali katika eneo la Rio na Mangueira , ili kuondoa magenge ya wahuni, taifa hilo linapojiandaa kuwa mwenyeji wa kombe la dunia la mpira wa miguu, miaka mitatu ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Mangueira, ni eneo lenye wakazi zaidi ya milioni moja, lililo karibu na uwanja wa mpira wa Maracana, sehemu maarufu zilipo shule za zamani za samba, dansi inayopendwa sana nchini humo.

Kwa mujibu wa maelezo ya wakazi wa eneo hilo, walengwa wa msako huo walitoroka eneo hilo kitambo, na kuongeza fedha hizo zilizopotea katika msako huo, zingekuwa na faida kubwa, iwapo zingekarabati hospitali na kuboresha huduma za afya.