Pakistani-Al Quaeda

Askari mmoja mwenye cheo cha Jenerali akamatwa nchini Pakistani.

Le général Athar Abbas, porte-parole de l'armée pakistanaise, lors d'une conférence de presse à Rawalpindi, le 12 octobre 2009.
Le général Athar Abbas, porte-parole de l'armée pakistanaise, lors d'une conférence de presse à Rawalpindi, le 12 octobre 2009. AFP

Msemaji wa jeshi la Pakistani Rawalpindi Athar Abbas amefahamisha kukamatwa kwa Jeneral moja wa jeshi nchini pakistani baada ya kushukiwa kushurikiana na kundi la kiislam lililopigwa marufuku nchini Humo.

Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo inatokea mwezi mmoja baada ya kutokea kifo cha marehem Osama Bin Laden, alieuawa na wanajeshi wa Marekani katika mji wa Abbottabad.

Kukamatwa kwa jenerali huyo kunaleta shuku kwamba baadhi ya wanajeshi wa Pakistani wanashirikiana na kundi la kiislam lenye fungamana na Al Qaeda.

Athar Abbas amesema uchunguzi umeanzishwa na serikali haitomvumilia yeyote yule ataekutwa na hatia ya kushirikiana na makundi yaliopigwa marufuku nchini pakistani.