Mamia ya wananchi wa mpakani mwa Syria na Uturuki wayatoroka makwao kwa kuhofia kuzuka machafuko

Wananchi wa Syria
Wananchi wa Syria REUTERS/Umit Bektas

Majeshi ya Serikali ya Syria yakiwa na vifaru yamerejea tene katika eneo la mpaka wa nchi hiyo ya Uturuki na kuchangia mamia ya wananchi kukimbia taifa hilo wakihofia huenda kukazuka machafuko kwa mara nyingine,huku umoja wa Ulaya ukipitisha vikwzo vipya kwa washirika wa rais Bashar Al -Asaad .

Matangazo ya kibiashara

Watu wanaokadiriwa kufikia mia sita wamekimbia Uturuki wakitoka Syria baada ya eneo la mpaka wa nchi hizo mbili kuvamia na majeshi ambao yanaendelea kuwasaka wale wanaopingana na serikali ya Rais Bashar Al Assad.

Wakati watu hao wakiwa wameshajitwali hifadhi kwenye Kijiji cha Guvecci taarifa zinaeleza mamia ya wananchi wameonekana wakiwa kwenye barabara wakikimbia kile ambacho kinatajwa ni operesheni ya kijeshi.

Eneo hilo la mpakani linadhaniwa kuwa na wanaharakati wengi ambao wamekuwa wakichochea kushinikizwa kwa mabadiliko ya kiutawala ambao wengi wanataka Rais Assad afanya mabadiliko ya kisiasa.

Operesheni hii inakuja baada ya hapo jana Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria kusema wamebaini Umoja wa Ulaya EU unahusika kwenye upangaji wa machafuko yanayoendelea kulitikisa taifa hilo.