CHINA

Rais Sudan Omar al-Bashir afanya mazungumzo na rais China, Hu Jintao

Rais Bashir, wakati akiwasili nchini China jana
Rais Bashir, wakati akiwasili nchini China jana Rueters路透社

Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, amekutana na rais wa China Hu Jintao mjini Beijing na kufanya mazungumzo.

Matangazo ya kibiashara

Rais Bashir ambaye aliwasili nchini humo siku ya jumanne anatarajiwa pia kukutana na waziri wa mafuta nchini humo na kufanya nae mazungumzo kuhusu uwekezaji wa nchi hiyo katika mafuta nchini Sudan.

Nchi ya China ni rafiki mkubwa wa serikali ya Sudan ambapo hununua zaidi ya nusu ya mafuta yanayozalishwa nchini humo.

Ziara ya rais Bashiri nchini China imeelezwa kuwa inalenga kutaka kuishawishi nchi ya hiyo kuendelea na uwekezaji wake nchini Sudan wakati huu ambapo Sudan Kusini inatarajiwa kujitenga na Kaskazini.

Tangu kupigwa kwa kura ya maoni nchini humo kuhusu Sudan Kusini kujitenga nchi ya China imeonekana kupunguza kasi ya uwekezaji na kuhofia kupoteza soko lake la mafuta nchini humo nchi hiyo ikijitenga.

Akizungumza mara baada ya kumpokea mgeni wake, rais Hu Jintao amesema kuwa ziara hiyo ni muhimu kwa mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa yakishirikiana kwa muda mrefu.

Licha ya rais Bashiri kutakiwa na mahakama ya kimataifa ya ICC amekuwa akifanya ziara mara kadhaa katika mataifa ambayo sio wanachama wa mahakama hiyo ikiwemo nchi ya China.