Iraq-Gagdad

Watu 10 wameuawa na wengine 28 wamejeruhiwa nchini Bagdad

eneo kuliko lipuka bomu
eneo kuliko lipuka bomu REUTERS/Mohammed Ameen

Watu 10 wamekufa na wengine zaidi ya 28 wamejeruhiwa nchini Iraq katika matukio mawili tofauti moja likiwa ni la bomu na jingine la kushambulia kwa risasi.

Matangazo ya kibiashara

Katika mji wa Baghdad watu wanne walipoteza maisha na wengine zaidi ya sita walijeruhiwa kufuatia shambulio la roketi katika eneo moja lenye ulinzi mkali jirani na hoteli moja ambayo hufikiwa na wageni kutoka nje ya nchi.

Msemaji wa polisi mjini Baghdad amesema kuwa shambulio hilo la roketi lilitekelezwa jirani na kituo cha mafuta ambapo kuna kituo cha polisi na hotoli na kuua watu wanne.

Wakati huohuo katika mji wa Kirkuk na Mosul watu watu zaidi ya sita wameripotiwa kufa katika matukio tofauti ya mabomu na kushambuliwa ka risasi matukio yanayokuja wakati ambapo vikosi vya kigeni vimetangaza kuondoa majeshi yao ifikapo mwishoni mwa mwaka 2012.