Watu zaidi ya 25 wauawa nchini Syria
Takriban waandamanaji 25 kadhaa wameuawa na vikosi vya nchini Syria hapo jana huku kukiwa na taarifa kuwa vifo hivyo vimetokea baada ya vikosi hivyo kuanzisha mashambulizi mjini Jisri al shughur karibu na mpaka wa nchi hiyo na uturuki.
Imechapishwa:
Hapo jana waandamanaji waliingia mitaani nchi nzima baada ya swalat l jumaa huku wakiimba nyimbo zao kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais wa nchi hiyo Bashar al Assad
Wanaharakati nchini humo waamesema mji huo sasa umekuwa mtupu baada ya wakazi wake takriban elfu hamsini kuukimbia mji huo na kwenda nchi jirani ya uturuki.
Hii leo marekani imekemea vikali machafuko ya nchini Syria hasa katika mji wa Jisr al shughur na kusema ni lazima uhalifu huo ukome haraka iwezekanavyo.