Thailand

Chama cha tawala zamani nchini Thailand kukifungulia mashtaka chama kilichonyakuwa uchaguzi

Mwanamama alieshinda uchaguzi
Mwanamama alieshinda uchaguzi Reuters

Chama cha democrats cha nchini Thailand kimefungua madai ya kisheria kukifungia chama cha pyu thai cha waziri mkuu wa zamani,Thaksini Shinawatra kilichokishinda demokrats kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa nafasi ya waziri mkuu,uchaguzi uliofanyika wiki iliyopita.hatua ambayo inahofiwa kusababisha kuanza upya kwa maandamano nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Mchakato huo unatarajiwa kuchukua miezi kadhaa kumalizika,hata hivyo hatua hiyo haimzuii waziri mkuu mpya Yingluck Shinawatra kutumikia wadhifa huo,hata kama chama hicho kikifungiwa kwa kuwa Yingluck si kiongozi wa chama.

Chama cha Democrat kimeitaka tume ya uchaguzi ya Thailand kufuatilia mchakato wa kukifungia chama cha thaksin Shinawatra kwa madai kuwa wanasiasa waliofungiwa kuhusika na maswala ya siasa walijihusisha na kampeni za chama hicho kabla ya uchaguzi uliofanyika jumapili.