Serikali ya Malaysia kukata huduma za usafiri na mji mkuu kuzuia waandamanaji wanaotaka mabadiliko
Polisi nchini Malaysia wamesema watafunga barabara kuu na kufunga huduma za usafiri wa uma kuelekea katikati ya mji wa kuala lumpour ili kuzuia wapinzani na wanaharakati waliopo kuendelea kuandamana kushinikiza mabadiliko ya sheria za uchaguzi.
Imechapishwa:
Vuguvugu hili la kisiasa limekuwa changamoto kubwa kwa waziri mkuu wa nchi hiyo,Najib Razak wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwakani.
Mkuu wa kikosi cha polisi Amar sin alitangaza jana jioni kuwa barabara kuu za kuingia mjini kuala lumpa zitafungwa kwa saa 22 kuanzia usiku wa manane hatua itakayoathiri huduma za usafirishaji na kuongeza kuwa tayari polisi wamepatiwa amri ya mahakama kuzuia wapinzani,makundi ya viongozi wa asasi za kiraia kuingia mjini humo.
Wanaharakati nchini humo wamesema wataendelea na maandamano bila kujali vitendo vya kukamatwa kwa raia na hofu ya kuzuka kwa vurumai.