Pakistani

Vikosi vya usalama nchini Pakistani vyaamrishwa kuwapiga risasi wamiliki wa silaha

Vikosi vya usalama vya nchini Pakistani hii leo vimeamrishwa kuwapiga risasi hadharani kundi la watu waliokuwa na silaha baada ya siku tatu za machafuko yaliyosababisha watu takriban sabini kupoteza maisha na kusababisha viongozi wa kisiasa kutenga siku ya maombolezo hatua iliyopelekea kufungwa kwa biashara mbalimbali na shuguli nyingine kusitishwa.

Majeshi ya Pakistani
Majeshi ya Pakistani REUTERS/Saeed Ali Achakzai
Matangazo ya kibiashara

Machafuko ya wiki hii ya mjini karachi yanaelezwa kuwa mabaya zaidi kutokea mwaka huu huku takriban watu thelathini na wanne wamepoteza maisha jana pekee,pale watu wenye silaha kufanya uharibifu wa mali.

Vyama vya Muttahida Qaumi na Awami National Party ,chama kinachowakilisha makundi mbalimbali ya kikabila ni vyama vinavyoshutumiwa kuhusika na vitendo vya mashambulizi mbalimbali yaliyofanyika nchini humo.