Syria

Maandamano yaendelea nchini Syria licha ya kuanza mazungumzo ya kitaifa

Waandamanji nchini Syria
Waandamanji nchini Syria Reuters

Maandamano zaidi yameendelea nchini Syria licha ya kuanza kwa mazungumzo ya kitaifa kati ya serikali na vyama vya upinzani nchini humo kujadili njia za kutafuta suluhu ya migogoro nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati mazungumzo hayo yakiendelea kumeripotiwa kifo cha mtu mmoja katika mji wa Homs kufuatia kuzuka kwa vurugu kati ya polisi na waandamanji katika mji huo ambao wanapinga mazungumzo hayo.

Siku ya jumapili mara baada ya serikali kufungua rasmi mazungumzo hayo ya kitaifa, chama kikuu cha upinzani nchini humo kilitishia kujitoa katika mazungumzo hayo kwa kile ilichodai lengo la mazungumzo hayo ni kujadili hali ya siasa na usalama nchini humo na sio masuala ya kijamii.

Ulinzi umendelea kuimarishwa katika miji mbalimbali nchini humo kufuatia kuanza kwa mazungumzo hayo.