Japani-Nyuklia

Waziri mkuu wa Japan atangaza mkakati mpya wa kuondokana na matumizi ya nishati ya umeme na nyuklia

Baada ya kuwa katika shinikizo la kujiuzuku na kuvunja baraza lake la mawaziri kwa miezi kadhaa, waziri mkuu wa Japan, Naoto Kan ametangaza mkakati mpya wa nchi yake wa kuondokana na matumizi ya nishati ya umeme inayotokana na Nyuklia.

Waziri mkuu wa Japani Naoto Kan
Waziri mkuu wa Japani Naoto Kan AFP PHOTO/Toru YAMANAKA
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza kupitia njia ya televisheni, waziri mkuu Kan amesema kuwa kwa kuhakikisha nchi yake haitegemei kuzalisha nguvu za umeme wa nyuklia kutafanya taifa hilo kuwa huru na kujiepusha na majanga kama yaliyoikumba nchi yao.

Kauli hiyo anaitoa wakati ambapo majuma kadhaa yaliyopita alitangaza mpango wa serikali yek wa kupitia upya uzalishaji wa umeme kwa kutumia nyuklia ambapo wamekubaliana kupunguza matumizi ya nguvu hizo kwa kiwango cha chini kabisa hadi kufikia mwaka 2030.