Umoja wa nchi za kiarabu waidhinisha uungwaji mkono wa Palestina kuwa mwenyekiti wa kudumu UN
Umoja wa nchi za kiarabu hapo jana uliidhinisha mpango wa Palestina kutafuta uanachama wa kudumu ndani ya Umoja wa Mataifa hali inayoelezwa kuwepo kwa upinzani mkubwa kati yake na Marekani ndani ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa iwapo nchi hiyo itapata nafasi hiyo.
Imechapishwa:
Mawaziri wa mambo ya nje ndani ya Umoja wa nchi za Kiarabu walikutana mjini Doha nchini Qatar na kuahidi kuisaidia Palestina katika hatua yao.
Mawaziri wameahidi katika taarifa yao kuwa watachukua hatua ya kushawishi nchi nyingine duniani hasa nchi wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa kuitambua Palestina na kupata nafasi ya kuwa mwanachama wa kudumu wa umoja wa mataifa.