INDIA-MUMBAI

Hofu ya usalama yatanda nchini India kufuatia ziara ya Hillary Clinton juma hili katika taifa hilo

Polisi wakikagua moja ya gari lililoharibiwa baada ya shambulio la bomu mjini Mumbai, India
Polisi wakikagua moja ya gari lililoharibiwa baada ya shambulio la bomu mjini Mumbai, India REUTERS/Stringer

Hali ya wasiwasi imeendelea kutanda nchini India siku chache kabla ya waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Hillary Clinton hajafanya ziara ya kikai nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Wakati kiongozi huyo akitarajiwa kufanya ziara juma hili, hofu ya kiusalama imeendelea kutanda nchini humo kufuatia juma lililopita kushuhudia milipuko mitatu ya mabomu mjini Mumbai iliyoua watu zaidi ya 17.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote lililodhibitisha kuhusika na shambulio hilo ingawa serikali ya India imekuwa ikiitupia lawama nchi ya Pakistan kwa kuhusika kifadhili vikundi vya mtandao wa kigaidi nchini humo tuhuma ambazo Pakistan imekanusha kuhusika nazo.

Waziri Clinton anataraiwa kuwasili nchini humo kesho ambapo atakuwa na mazunguzmo na waziri mkuu Manmohan Sighn siku ya jumanne huku usalama ukiimarishwa kufuatia ziara hiyo.