Bahreini

Chama kikuu cha upinzani nchini Bahreini cha jiondowa katika mazungumzo na serikali

Chama kikuu cha upinzani nchini Bahrain cha Wefaq kimetangaza rasmi kujitoa katika mazungumzo ya kitaifa yaliyoitishwa na serikali ya nchi hiyo kujadili hali ya kisiasa nchini humo.

Ali Salmane, Mkuu wa kundi la upinzani e Al Wefaq
Ali Salmane, Mkuu wa kundi la upinzani e Al Wefaq REUTERS/Hamad I Mohammed
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa chama hicho Kjalil al-Marzouk amesema kuwa kamati ya juu ya chama hicho imeamua kufikia uamuzi huo baada ya kuona mazungumzo hayo hayana mafanikio na serikali kupuuza wito ambao chama chao imekuwa ikiutoa kuhusu malengo rasmi ya majadiliano hayo.

Juma lililopita chama hicho kilidai kuwa mazungumzo hayo hayalengi kutatua mgogoro wa kisiasa na kiusalama unaoikumba nchi hiyo badala yake umekuwa ukijadili masuala ya kijamii ambayo hayakuwa malengo ya awali ya kuanzishwa kwa mazungumzo hayo.

Tayari kiongozi wa chama hicho Sheikh Ali Salman ametangaza chama chake kufanya maandano makubwa nchini humo juma hili kushinikiza kufanyika mabadiliko ya kidemokrasia nchini humo.