China-Ajali
Familia za watu waliopoteza watu katika ajali ya garimoshi nchini China wakataa fidia
Imechapishwa:
Familia zilizopoteza wapendwa wao katika ajali ya garimoshi, nchini China hivi karibuni, zimekataa fedha za fidia mpaka hapo chanzo cha ajali hiyo, kitakapowekwa bayana.
Matangazo ya kibiashara
Kwa mujibu wa gazeti la China Daily, familia hizo zimefikia hatua hiyo kutokana na kutoridhishwa na namna maofisa wa serikali wanavyoshughulikia uchunguzi wa ajali hiyo.
Mmoja wa wanafamilia hao Wang Hui, amesema wanachohitaji wao si fedha bali ukweli, juu ya ajali hiyo.
Na Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao amesisitiza kufanyika kwa uchunguzi makini wa ajali hiyo ya jumamosi, iliyosababisha watu thelathini na tisa kupoteza maisha.