JAPANI

Chama Kikuu cha Upinzani Nchini Japani LDP kimemtaka Waziri wa Ulinzi ajiuzulu

Reuters路透社

Chama Kikuu cha Upinzani Nchini Japan cha LDP kimetaka Waziri Mpya wa Ulinzi nchini humo Yasuo Ichikawa mbaye hata hajaapishwa rasmi aandoke madarakani baada ya kujitamba hadharani yeye si mtu aliyebobea kwenye masuala ya ulinzi.

Matangazo ya kibiashara

Ichikawa aliviambia vyombo vya habari kabla ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo kuwa yeye hana ujuzi kwenye sekta ya ulinzi kitu ambacho kinasimamiwa na Chama Cha LDP kuwa ni kigezo cha Waziri huyo mpya kuondoka kwenye ofisi hiyo.

Mkuu wa Sera wa Chama Cha LDP ambaye ni Waziri wa zamani wa Ulinzi Shigeru Ishiba amesema ni hatari kwa suala kama la usalama na ulinzi kuweka kwenye mikono ya mtu ambaye si mjuzi kwenye maeneo hayo.

Ishiba amesema hata busara ambayo imetumika na Waziri Mkuu Yoshihiko Noda kumchagua Ichikawa kuwa Waziri wa Ulinzi ni kitu ambacho kinastahili kuhojiwa na kunaibua maswali mengi kwa wananchi.

Chama hicho Kikuu cha Upinzani cha LDP kimesema maneno hayo yanatosha kabisa kumfanya Waziri Ichikawa kuondoka au kuondolewa kwenye wadhifa wake huo ambao anatarajiwa kuapishwa na kuutumikia.

Ichikawa ambaye amekuwa akihudumu kwenye Wizara ya Kilimo kama mtaalam kwa miaka ishirini na tano kabla ya kuingia kwenye uga wa kisiasa na tayari mwenyewe amesema kauli yake ilitafsiriwa vibaya.

Waziri huyo wa Ulinzi amesema alichokuwa anamaanisha yeye ni kwamba wananchi wengi ndiyo hawana ujuzi wa masuala ya Ulinzi na Usalama kwa hiyo serikali inawajibu wa kuibuka na sera ambayo itawafungua raia kimtazamo.

Huu ni mtihani wa kwanza kwa Waziri Mkuu Noda ambaye amekuwa Waziri Mkuu wa Sita wa Japan katika kipindi cha miaka mitano huku pia akitakiwa kukabiliana na changamoto mbalimbali zikiwemo kuimarisha uchumi wa taifa hilo.