INDIA

Mwanaharakati wa india Anna Hazare aahidi shinikizo zaidi kwa serikali hadi ichukue hatua kupambana na rushwa

Mwanaharakati Mahiri wa kupambana na Vitendo vya Ulaji wa Rushwa nchini India Anna Hazare amesema wanaendelea na harakati zao wakifanya matukio ya kushtua hadi pale ambapo serikali ya nchi hiyo itakapokuwa tayari kuondoa kabisa tatizo la rushwa.

Matangazo ya kibiashara

Hazare ametoa kauli hiyo wakati aliporejea Kijiji mwake Ralehan Siddhi kilichopo katika Jimbo la Maharashtra baada ya kutumia muda wa zaidi ya majuma mawili akiwa New Delhi ambapo alikuwa anatekeleza ahadi yake ya kujizuia kula na kunywa.

Mwanaharakati huyo akiwa amezungukwa na wafuasi wake wanaokadiriwa kufikia elfu moja amewaambia serikali lazima itambue wataendelea kutekeleza matukio mbalimbali ikiwa ni njia ya kuwashtua na kusikiliza kilio chao cha kumaliza rushwa Nchini India.

Hazare amesema inasikitisha sana kuona nchini ya India inaadhimisha miaka 64 ya uhuru iliyoupata kutoka kwa Wakoloni wao Uingereza lakini hakuna mabadiliko yoyote ambayo yamefanyika kwenye taifa hilo.

Mwanaharakati huyo amatuma salamu kwa vijana wa nchi hiyo kuwa wawe tayari kwenda jela pindi watakapokuwa wanahudhuria mikutano yake ya kufanikisha kupambana na vitendo vya ulaji wa rushwa.

Kiongozi huyo wa harakati za kukabiliana na vitendo vya rushwa nchini India amesema hakuna shida kwa yoyote kwenda jela kwa kuwa anendelea kupata huduma zote ikiwemo milo mitatu kwa siku.

Hazare bila ya kuwa na hofu yoyote amelishukia Bunge la Congress nchini India na kusema halina nia dhati ya kukabiliana na kuondoa rushwa ambayo imeshika kasi katika eneo la nchi hiyo kutokana na kutokuwepo sera madhubuti.

Mwanaharakati huyo alisitisha mpango wake wa kuendelea kutia mgomo wa kula na kunywa baada ya Wabunge nchini India kuridhia kufanyikazi mapendekezo yake ambayo alikuwa ameyatoa kwa serikali.

Anna Hazare amekuwa mwanaharakati maarufu sana nchini india huku wengi wakimfananisha na Mpigania uhuru maarufu wa taifa hilo Mahatma Gandhi kutoka na misimamo ambayo anayo.