Bingwa wa mchezo wa masumbwi nchini Phillipine atangaza nia ya kustaafu na kuwania umakamu wa rais

RFI

Bingwa wa mchezo wa masumbwi duniani, Manny Pacquiao ambae ni raia wa Phillipines ametagaza kuwa anataka kustaafu katika mchezo huo, na kuwania umakamu wa urais, kwa muda miaka mitano ijayo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo wachambuzi wa maswala ya kisiasa nchini humo wanasema kuwa itakuwa vigumu mno kikatiba kwa mwanabondia huyo kuwania wadhifa huo ,mwaka 2016 kwa sababu ya umri wake.

Kufikia mwaka 2016, wakati wa uchaguzi huo, bondia huyo atakuwa na umri wa miaka 37, na hivyo atafungiwa nje ya kinyanganyiro hicho, kwa sababu hatakuwa amefikisha umri wa miaka 40 na zaidi kama katiba inavyotakiwa kikatiba.