Syria

Mahujaji 22 wakishiha, wauawa wakati wakiwa safarini nchini Syria

rian

Takriban abiria 22 waliokuwa wakisafiri kwa basi kutoka Iraq kulekea Syria katika jimbo la Anbar lililo magaharibi mwa Iraq wameuawa na watu wenye silaha jana.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea katika eneo lenye umbali wa kilometa 300 magharibi mwa mji wa Baghdad eneo lililo chini ya majeshi ya Iraq. Watu wenye silaha walijitokeza na kuwauawa watu hao ambao ni mahujaji wa kishiha waliokuwa wakielekea nchini Syria.

Polisi imesema kuanzisha operesheni ya kuwasaka wahusika wa tukio hillo la mauaji.

Tangu operesheni ya vikosi vya kigeni kuingia nchini Iraq mwaka 2003, jimbo la Anbar lenye raia wa madhehebu ya Sunni limekuwa likidhibitiwa na makundi ya kigaidi ya Al Qaeda, ambalo limeua raia wengi wa Iraq na wageni waliokuwa wakisafiri katika barabara za Jordan na Syria.

Pamoja na jitihada za wapiganaji wa jadi kupambana na makundi ya kigaidi mwaka 2007 hawajafanikiwa kuyaondoa makundi hayo mpaka sasa.