Yemeni

Mapigano mapya yazuka katika jiji la Sanaa nchini Yemeni

Mapigano kati ya wafuasi wa rais wa Yemeni Ali Abdallah Saleh na wapinzani.
Mapigano kati ya wafuasi wa rais wa Yemeni Ali Abdallah Saleh na wapinzani. Reuters/Khaled Abdullah

Mapigano mapya yamezuka tena katika mji wa Sanaa nchini Yemen, kati ya wanadamanaji na majeshi ya serikali licha ya makubaliano ya kusitisha mapigano hayo.

Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji watatu, wameuawa leo baada ya kukabiliana na polisi mjini Sanaa, huku zaidi ya wengine 25 wakijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini.

Waaandamanaji nchini Yemen, wanataka kumalizika kwa uongozi wa rais wa nchi hiyo Ali Abdula Saleh amabye ameongoza nchi huyo tangu mwaka 1978 na kwa sasa yuko Saudi Arabia anakopata nafuu baada ya kushambuliwa mwezi Juni mwaka huu.