Yemeni

watu 16 wauawa nchini Yemeni wakati wakiwa mazikoni

Maandamano mjini Sanaa
Maandamano mjini Sanaa REUTERS/Khaled Abdullah

watu kumi na sita wameuawa na vikosi vya usalama nchini Yemen wakati maelfu ya raia walipofyatuliwa risasi waliokuwa kwenye shughuli za mazishi ya waandamanaji waliouawa katika mapambano.

Matangazo ya kibiashara

Waombolezaji walikusanyika kwa ajili ya maziko ya waliouawa katika mapambano ya siku tatu mfulululizo ambapo idadi ya waliopoteza maisha imefikia takriban watu 80 mpaka sasa.

kuongezeka kwa machafuko hayo kimesababishwa na kile kinachoswemwa na waandamanaji kuwa wamechoshwa na rais wa nchi hiyo Ali Abdullah Salleh kwa kuwa amekuwa akichelewesha kutia saini mapendekezo yatakayomfanya aondoke madarakani.