Pata taarifa kuu
Ufilipino

Idadi ya watu walioathiriwa na kimbunga nchini Ufulipino yafikia elfu 65

Watoto Nchini Ufilipino wakitoka chuoni wakati mvua kubwa ikinyesha Septemba 26.2011.
Watoto Nchini Ufilipino wakitoka chuoni wakati mvua kubwa ikinyesha Septemba 26.2011. REUTERS/Cheryl Ravelo
Ujumbe kutoka: Ali Bilali
Dakika 1

Serikali ya nchini Ufilipino imeanza kuwawezesha waathirika kwa kuandaa harakati za kuwapa fidia ya makazi yao, pamoja na ukarabati wa maeneo yote yaliyoathiriwa na kimbunga cha Nesat kilichoikumba nchi hiyo hivi karibuni.

Matangazo ya kibiashara

Wakati jitihada hizo zikiendelea imeripotiwa ongezeko la vifo na kufikia watu 18, ambapo vikosi vya uokozi vinajitahidi kuokoa lakini bado zaidi ya watu 35 hawajulikani walipo kufuatia kimbunga kilichoambatana na upepo mkali na mvua.

Wakala wa dharura wa nchini Ufilipino amesema kuwa zaidi ya watu elfu 65 wamesambazwa katika vituo vilivyotengwa kwa ajili ya watu waliopoteza makazi ili kungojea utaratibu wa kupatiwa fidia ya makazi yao.

Hii ni mara nyingine ambapo nchi ya Ufilipino imekumbwa na kimbunga ambapo katika miaka 2 iliyopita kimbunga cha ketsana kiliipiga nchi hiyo na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 400.
 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.