MYANMAR

Serikali ya Myanmar yatoa msamaha kwa wafungwa zaidi ya 6,000

Serikali ya Myanmar imetangaza msamaha kwa maelfu ya wafungwa nchini humo kwa ajili ya kurejesha matumaini kwa wanasiasa ambao wamekuwa hawana imani na uatawala wa kijeshi ambao umekaa madarakani kwa muda mrefu kabla ya kufanyika uchaguzi.

Soe Zeya Tun/ Reuters
Matangazo ya kibiashara

Myanmar inakadiriwa kuwa na wafungwa wa kisiasa zaidi ya elfu mbili wakiwemo wale ambao wanashinikiza demokarasia nchini humo, waandishi wa habari na wanasheriakitu ambacho kiliyafanya Mataifa ya Magharibi kuiwekea vikwazo nchi hiyo.

Kwa mujibu wa tangazo hilo lililotolewa kwenye Televisheni ya Taifa hilo linaeleza wafungwa elfu sita mia tatu wakiwemo wagongwa, vikongwe, walemavu na wafungwa watiifu watapata msamaha huo wa serikali.

Tangazo hilo limeshindwa kuanisha iwapo wafungwa wakisiasa nao watakuwa ni miongoni mwa wale ambao watapewa msamaha na serikali wakati hili kiliwa zoezi la kwanza la namna hiyo kufanywa.

Maelezo zaidi ya tangazo hilo wanaweka bayana uamuzi wa serikali wa kuwaachia wafungwa hao unalengo la kutaka kurejesha mshikamano pamoja na kuijenga Myanmar mpya kwa maendeleo na manufaa ya nchi.

Taarifa hizi zimekuja saa kadhaa baada ya serikali kuchagua Jopo la Serikali ambalo litashughulikia masuala ya Haki za Binadamu ambalo limeahidi kushughulikia malalamiko ya wafungwa yaliyopo.

Takwimu ambazo zimetolewa na Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International limesema hukumu nyingi za wafungwa nchini Myanmar si za haki kwani wengi wanatuhumiwa kwa makosa ya ukatili.

Uamuzi huo wa msamaha kwa wafungwa umepokelewa kwa mikono miwili na wapinzani nchini Myanmar ikiwemo Chama Kikuu cha Upinzani cha NLD ambacho kilishuhudia Aung San Suu Kyi akitumia kifungo cha ndani kwa miaka saba.

Msemaji wa Suu Kyi, Nyan Win amesema hiyo ni hatua nzuri lakini hawajapewa taarifa iwapo wanachama wao ambao wamefungwa kama watakuwemo miongoni mwa wafungwa watakaoachiwa.