Korea

Kiongozi wa UN wa maswala ya kibinadamu azuru korea kaskazini

ESSENTIEL

Kiongozi wa maswala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Valerie Amos yuko nchini Korea Kaskazini, kutathmini kiwango cha chakula katika taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Katika ziara hiyo, Amos anashauriana na viongozi wa serikali ya Korea Kaskazini namna mbinu za umoja huo za kuongeza misaada ya vyakula nchini humo, hasa baada ya taifa hilo kukumbwa na janga la njaa katika miaka ya tisini na kusabisha maelfu ya watu kupoteza maisha yao.

Kwa muda mrefu sasa, serikali ya Pyongyang kwa muda mrefu sasa imekuwa ikitegemea vyakula vya msaasa kutoka umoja huo wa umoja wa mataifa kuwalisha wananchi wake.

Umoja wa mataifa unasema kuwa, zaidi ya watu milioni sita nchini Korea Kaskazini wanahitaji chakula.