KOREA KASKAZINI

Utafiti waonyesha vyombo vya habari vya kimataifa kuanza kupewa nafasi nchini Korea Kaskazini

Askari wa Korea Kusini akiwa amesimama kwenye eneo ambalo nchi hiyo ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu
Askari wa Korea Kusini akiwa amesimama kwenye eneo ambalo nchi hiyo ilifanya jaribio la kombora la masafa marefu REUTERS/Bobby Yip

Utafiti mpya uliofanywa nchini Korea Kaskazini kuhusu vyombo vya habari umeonesha kuwa vyombo vya habari vya kimataifa vimeanza kupata nafasi ya kuingia nchini humo kutoa habari.

Matangazo ya kibiashara

Nchi hiyo ambayo awali ilikuwa inatajwa kama moja ya nchi amabyo haina uhuru wa vyombo vya habari, hivi sasa inatajwa kama moja ya nchi ambayo vyombo vya habari vya kimataifa vimeanza kupata nafasi nchini humo.

Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na kituo kimoja cha nchini Marekani, imesema kuwa tamthilia nyingi na michezo ya kuigiza inayoingia nchini humo imetokea kwa majirani zao Korea Kusini.

Ripoti hiyo imeongeza kuwa picha nyingi za video zimeingizwa nchini humo kupitia kwenye mpaka wa nchi hizo mbili na kwa usiri mkubwa.

Hivi karibuni kwa mara ya kwanza Serikali ya nchi hiyo iliruhusu vyombo vya habari vya kimataifa kuingia nchini humo kupiga picha tukio nchi hiyo wakati ikifanya majaribio ya kurusha kombora lake la masafa marefu ambalo hata hivyo lilishindikana.