AFGHANISTAN

Watu watatu wauawa katika shambulizi lililotekelezwa na kundi la Taliban nchini Afghanistani

REUTERS

Takribani watu watatu wameuawa na wengine saba kujeruhiwa leo jumatano kufuatia shambulio la bomu lililotekelezwa katika kambi ya majeshi ya Marekani iliyopo mashariki mwa Afghanistani.

Matangazo ya kibiashara

Kundi la wanamgambo wa Taliban ambalo limekuwa likihusishwa na mashambulizi dhidi ya wageni na majeshi ya serikali kwa zaidi ya muongo mmoja limejigamba kuhusika na tukio hilo.
 

Shambulio hilo linakuja siku mbili baada ya polisi mwanamke wa Afghanistani kumpiga risasi na kumuua Mshauri wa vikosi vya kujihami vya nchi za magharibi NATO katika ofisi za makao makuu ya polisi mjini Kabul.

Vikosi vya NATO vipo katika mkakati wa kuondoka nchini Afghanistani na vitaondoa vikosi vyake 100,000 mwaka 2014.

Kumekuwa na hofu kuwa huenda kukaibuka vita baada ya NATO kujiondoa nchini humo kutokana na vikosi vyake kutoa msaada kwa serikali katika kukabiliana na wapiganaji wa Talibani.