Pata taarifa kuu
INDIA

Maadamano yazidi kupamba moto baada ya serikali ya India kuunda Tume ya kuchunguza vitendo vya ubakaji

©Reuters.
Ujumbe kutoka: Flora Martin Mwano
1 Dakika

Serikali ya India imeagiza uchunguzi wa kina ufanyike kutokana na kuibuka kwa maandamano na ghasia za kutaka kuchukuliwa hatua kali kwa wabakaji wa mwanafunzi wa udaktari tarehe 16 ya mwezi huu. Wakati huo huo waandamanaji nao wameendelea na harakati za kushinikiza serikali kutoa adhabu ya kifo kwa waliohusika na kitendo hicho.

Matangazo ya kibiashara

Serikali imeunda Tume Maalum ambayo itafanya kazi ya kudadisi chanzo cha tukio hilo na uwepo wa matukio ya ubakaji ambayo yanatajwa kuchangia hofu ya usalama kwa wanawake wa Taifa hilo.

Waziri wa Fedha wa India na Msemaji wa Serikali Palaniappan Chidambaram amesema watahakikisha mabadiliko ya sheria kwa wabakaji nayo yanafanyika baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.

Wakati serikali ikiwa katika mchakato huo Mwanafunzi aliyebakwa akiwa ndani ya basi amewasili nchini Singapore leo alhamisi kwa matibabu zaidi.

Duru za kitabibu zimeeleza kuwa Mwanafunzi huyo tayari ameishafanyiwa oparesheni tatu akiwa India baada ya kuathiriwa vibaya na ubakaji huo aliofanyiwa tarehe 16 mwezi huu.

Serikali ya India ambayo inafadhili gharama za matibabu huyo imethibitisha kumsafirisha Mwanafunzi mpaka katika hospitali ya Mount Elizabeth ya Singapore ambapo anaendelea kupatiwa matibabu kwa sasa.

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.