Korea ya kusini

Rais wa kwanza Mwanamke nchini Korea kusini aapishwa

Rais wa kwanza mwanamke nchini Korea Kusini Park Geun-Hye ameapishwa leo jijini Seoul katika sherehe iliyohudhuriwa maelfu ya raia wa taifa hilo.

Rais wa Korea kusini, Park Geun-Hye
Rais wa Korea kusini, Park Geun-Hye
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo mpya ameahidi kuinua uchumi wa taifa hilo pamoja na kuwaahidi raia wake usalama na kusisitiza kuwa serikali yake haitatishwa na vitisho kutoka kwa jirani zao Korea Kaskazini.
 

Rais huyo pia ameahidi kuhakikisha kuwa ajira zinaundwa nchini humo ili taifa hili liendelee kiuchumi na raia wake kuishi maisha mazuri.
 

Rais Park Geun-Hye mwenye umri wa miaka 61 amekiri kuwa hayo ndio mambo makubwa ambayo raia wake wanatarajia kutoka kwake kama kiongozi wa atatekeleza kama kionhgozi wa nne wa taifa hilo.
 

Park ameitaka serikali ya Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa Nuklia ili kushirikiana na matifa mengine duniani .
 

Baba yake Rais Park, mwanjeshi Park Chung-He aliwahi kuongoza taifa hilo kwa miaka 18 miaka hamsini iliyopita kabla ya kuuawa.