Kazakhstani

Mazungumzo kati ya Mataifa yenye nguvu duniani na Iran yakamilika

Mkutano wa wajumbe wa Mataifa yenye nguvu duniani na nchi ya Iran
Mkutano wa wajumbe wa Mataifa yenye nguvu duniani na nchi ya Iran Reuters / Omarov

Mataifa yenye nguvu duniani na Iran wamekamilisha mazungumzo ya siku mbili nchini Kazakhstani yaliyolenga kujadili mpango wa Nuklia wa Iran hata hivyo hakuna ishara yeyyote inayoonesha kuwa walifikia makubaliano.

Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo Marekani, Urusi, China, Uingereza, Ufaransa na Ujerumani walionesha kuridhishwa kwa hatua ya kufanyika kwa mazungumzo yakisema ni ya msingi.
 

Siku ya pili ya mazungumzo ilihusisha mazungumzo ya ana kwa ana kati ya Mkuu wa Sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton na Mjumbe Mkuu kutoka Iran, Saeed Jalili.
 

Afisa kutoka nchini Iran pia amethibitisha kuwa mazungumzo yamekamilika na kuwa Taarifa zaidi juu ya Mazungumzo hayo zitatolewa.
 

Mataifa yenye nguvu duniani yalikubaliana kupunguza makali ya Vikwazo dhidi ya Iran huku ikiitaka Iran kupunguza kiwango chake cha urutubishaji wa Madini ya Uranium.
 

Ashton amesema kuwa sasa ni juu ya Iran kuridhia hatua ya Mataifa hayo huku Iran nayo ikisema kuwa itakuja na Maazimio yake.