Afghanistani

Watu sita wajeruhiwa kwa Shambulizi la kujitoa muhanga

Rais wa Afghanistani Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani Hamid Karzai REUTERS/Omar Sobhani

Watu sita wamejeruhiwa baada ya mtu mmoja anayeelezwa kuwa mfuasi wa kundi la Wanamgambo wa Taliban kujitoa muhanga akilenga basi lililokuwa limebeba Wanajeshi wa nchini Afghanistani mjini Kabul.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo la bomu la kujitoa muhanga limetekelezwa katika mtaa ambao uko kwenye ulinzi mkali ambapo wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakikiri kufanya mashambulizi ya kujitoa muhanga wakiwalenga Maafiasa wa Idara ya intelijensia na makao makuu ya Polisi mwaka huu.
 

Mashambulizi haya yanakuja wakati ambapo Vikosi vya NATO vikijiandaa kuondoka nchini Afghanistani na kuachia Vikosi vya Afghanistani majukumu ya kulinda usalama.
 

Idadi ya Mashambulizi ya Wanamgambo mwaka 2012 imeonesha kuwa imeendelea kuongezeka nchini humo.
 

Marekani na NATO inawanajeshi Takriban 100,000 nchini Afghanistan lakini wengi wao wataondoka nchini humo ifikapo mwaka ujao.