KOREA KASKAZINI

Korea Kaskazini yaionya Kusini juu ya kisiwa chenye mgogoro

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-Un ameionya jirani yake Korea Kusini kuwa itafanya mashambulizi katika kisiwa kinachogombaniwa cha Baengnyeong, tishio hilo linaendeleza kudora kwa uhusiano kati ya nchi hizo mbili.

REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Akiwa katika ziara yake katika eneo la mpaka Kim amekitaja kisiwa cha Baengnyeong kama kitovu cha mgogoro wa mataifa hayo.

Tishio hili linakuja siku moja baada ya wanajeshi wa Marekani na wale wa Korea Kusini kuanza kuyafanya mazoezi ya pamoja na kujiweka tayari kwa mashambulizi kutoka Pyongyang.

Siku kadhaa zilizopita Korea Kaskazini ilitishia kushambulia Korea Kusini na Marekani baada ya Umoja wa Mataifa UN kuiwekea vikwazo kutokana na Taifa hilo kutekeleza jaribio lake la tatu la nyuklia mwezi uliopita.

Katika hatua nyingine Shirika la umoja wa Mataifa linaloshughulika na haki za binadamu linataka Umoja wa Mtaifa kupitia baraza lake la usalama kufanya uchunguzi wa ukiukwaji wa haki za binadamu nchini Korea Kaskaini kuanzia mwaka 2004.