PAKISTAN

Mahakama nchini Pakistan yatoa agizo la kukamatwa kwa Pervez Musharraf

Mahakama nchini Pakistan imeamuru kukamatwa kwa kiongozi  wa zamani wa nchi hiyo Pervez Musharraf kutokana na hatua yake ya kuwapa Majaji kifungo cha nyumbani mwaka 2007.

Matangazo ya kibiashara

Musharraf alikuwa Mahakamani wakati agizo hilo lililotolewa wakati alipokuwa amefika katika Mahakama hiyo kuomba dhamana kuhusu kesi hiyo.

Hata hivyo, polisi hawakumkamata wakati agizo hilo lilipototelewa na Mahakama hiyo na kiongozi huyo wa zamani wa kijeshi aliondoka katika Mahakama hiyo akiwa amezingizwa na walinzi wake.

Mawakili wake wanasema kuwa mteja wao ana haki ya kukata rufaa kuhusu agizo hilo la Mahakama.

Agizo hili linakuja siku chache tu baada ya tume ya uchaguzi nchini humo kumfungia kutoshiriki kwa namna yeyote kuhusu uchaguzi Mkuu mwaka huu.

Musharaf alirudi nyumbani mwezi uliopita kutoka Dubai alikokuwa anaishi, na kusema kuwa amerudi nyumbani ili kuikoa Pakistan.

Kiongozi huyo wa zamani pia anakabiliwa na kesi mbalimali ikiwemo ya uhaini huku, kundi la kigaidi la Taliban ambalo limeendelea kupinga serikali nchini humo ikisema inalenga kumshambulia.

Mussaraf mwenye umri wa miaka 69 alikuwa rais wa kumi wa nchi hiyo kati ya mwaka 2001 hadi 2008 kabla ya kujiuzulu na kukimbilia ukimbozini jijini London nchini Uingereza.

Wakati tangazo hilo likitolewa, watu wanne wameuawa baada ya msafara wa upinzani wa chama cha PML-N kuvamiwa Kusini Magharibi mwa nchi hiyo.