Afghanistani

Madhara kwa Raia wa Afghanistani kutokana na Mashambulizi ya Wanamgambo yafikia asilimia 30 kwa kipindi cha miezi mitatu ya kwanza

Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakihatarisha usalama wa Afghanistani hata baada ya vita ya miaka 10 ya kusambaratishwa kwao
Wanamgambo wa Taliban wamekuwa wakihatarisha usalama wa Afghanistani hata baada ya vita ya miaka 10 ya kusambaratishwa kwao REUTERS

Madhara kwa Raia yatokanayo na mashambulizi nchini Afghanistan yameongezeka kufikia asilimia 30 katika kipindi cha miezi mitatu ya kwanza mwaka huu, mjumbe wa Umoja wa Mataifa ameeleza akilitaja shambulio la hivi karibuni lililotekelezwa na kundi la wanamgambo wa Taliban kuwa ni uhalifu wa kivita.

Matangazo ya kibiashara

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan Jan Kubis amesema Raia 475 waliuawa na wengine 872 walijeruhiwa tangu mwezi Januari mpaka Machi.
 

Kubis ametoa wito kwa makundi yanayopambana na Serikali ya Afghanistani kuacha kuwashambulia Raia , kuwatumia Watoto katika mashambulizi ya kujitoa muhanga na kushambulia maeneo yenye watu wengi yakiwemo maeneo ya kufanyia ibada.
 

Akizungumzia Shambulio la Aprili 3 dhidi ya jengo la mahakama magharibi mwa mji wa Farah na kauli ya Taliban kuwa hivi sasa wanalenga mahakama za nchini humo, Kubis ameeleza kuwa ni jambo la kuangaliwa kwa karibu sana.
 

Wafuasi wa Taliban wakiwa na Silaha waliwaua watu 46 wakiwemo raia 36 katika jengo la Mahakama ili kuwatorosha Wanamgambo waliokuwa katika eneo hilo kwa ajiki ya kusikiliza kesi zao.
 

Kubis ametoa wito kwa Vikosi vya Afganistan na vya jumuia ya kujihami ya nchi za Magharibi NATO kuchukua hatua za kulinda Raia na kufanyia uchunguzi vitendo hivyo.