Korea kaskazini

Korea kaskazini yakataa pendekezo la Korea kusini kufanya Mazungumzo

Rais wa Korea kaskazini, Kim Jong Un
Rais wa Korea kaskazini, Kim Jong Un

Korea kaskazini imekataa ombi la Korea kusini la kufanya mazungumzo iliyoyaita ya kinafiki juu ya kuanza tena kwa shughuli za pamoja za uzalishaji katika viwanda na kuitaka Seoul kuondoa Wafanyakazi wake wote waliobaki katika eneo la Kiwanda.

Matangazo ya kibiashara

Korea kusini iliipa Korea kaskazini saa 24 kukubali kufanya mazungumzo juu ya Mustakabali wa kiwanda cha Kaesong na kuonya kuwa itachukua hatua ikiwa Pyongyang itakataa.
 

Ikitupilia mbali wito huo uliotolewa na Seoul, Korea kaskazini imetupa lawama kwa Korea kuosini kuwa imekuwa chanzo cha mgogoro katika kiwanda hicho na kuwa kuweka zaidi Masharti hakujengi lolote isipokuwa kuweka mvutano huo katika hali mbaya zaidi.
 

Peninsula ya Korea imeingia katika mgogoro baada ya hatua ya Korea kaskazini kufanya jaribio lake la Nuklia mwezi Februari na kuzuia Korea kusini kushiriki katika uzalishaji katika eneo la Viwanda vya Kaesong.
 

Viwanda vya Korea kusini ambavyo vinafanya kazi katika eneo la viwanda vya Kaesong wameapa kuendelea kubaki katika eneo hilo na kutetea maslahi na kupigania haki yao bila kujali hatua ambayo Serikali ya Seoul itachukua.
 

Pamoja na mvutano uliokuwepo kati ya mataifa hayo mawilli, uamuzi wa Kaskazini kusitisha Shughuli za viwanda haukutarajiwa, na kuwa mataifa hayo mawili hayakutarajia mgogoro huo ungeathiri viwanda vya pamoja.
 

Kufungwa kwa eneo la viwanda kutaathiri chanzo cha mwasiliano ambayo yalikuwa yamebaki kati ya nchi hizo.