MALAYSIA

Wamalaysia wapiga kura katika uchaguzi wa kwanza wa kihistoria

Wapiga kura wakiwa kwenye msitari wakingoja kupiga kura zao
Wapiga kura wakiwa kwenye msitari wakingoja kupiga kura zao malaysia.com

Wananchi wa Malasyia wanapiga kura leo Jumapili katika uchaguzi wa kwanza katika historia ya taifa hilo huku mabadiliko ya serikali yakiwa hatarini ambapo serikali inayomaliza muda wake inapambana kuzuia ukuaji wa upinzani unaotishia kufanya mageuzi. 

Matangazo ya kibiashara

Zoezi la upigaji kura limeanza majira ya asubuhi ambapo zaidi ya vituo elfu nane vya kupigia kura vimefunguliwa nchi nzima huku mvutano ukiwa juu baada ya kampeni ya uchungu iliyotawaliwa na mashitaka ya wapinzani kuhusu udanganyifu na kuenea kwa vurugu kumalizika hapo jana.

Serikali iliyopo madarakani chini ya Chama tawala cha United Malays National Organisation ni moja ya Serikali iliyodumu kwa muda mrefu duniani na haijawahi kutishwa tangu uhuru mwaka 1957.