MYANMAR

Boti za Rohingya za zama Magharibi mwa Myanmar, wanane wafariki

Abiria wakiwa ndani ya boti
Abiria wakiwa ndani ya boti presstv.ir

Boti kadhaa za abiria zilizokuwa zimewabeba waisilamu wenye asili ya Rohingya nchini Myanmar, zimezama Magharibi mwa nchi hiyo na kusababisha kupotea kwa abiria wengi.

Matangazo ya kibiashara

Boti hizi zilikuwa zimewabeba zaidi ya abiria miamoja waliokuwa wanakimbia kimbunga kikubwa katika jimbo la Rakhine.

Maafisa wa uokoaji nchini humo wamesema kuwa hadi sasa wamefanikiwa kuwaokoa abiria wapatao arobaini pamoja na miili minane.

Maelfu ya waumini wa Rohingya wamekuwa wakiishi katika jimbo la Rakhine tangu mwaka uliopita kutokana na machafuko yaliyozuka dhidi yao na kusababisha maelfu ya watu kukimbia makazi yao.

Umoja wa mataifa unasema kuwa msaada wa haraka unahitajika kuwafikia waathiriwa wote wa mkasa huo  pamoja na raia wengine wa nchi hiyo ambao walikimbia makwao kutokana na mafuriko ya mwaka uliopita.