PAKISTANI

Waziri mkuu wa Pakistan aapa kushirikiana na mataifa ya Magharibi kwa maendeleo ya taifa lake

Waziri mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif
Waziri mkuu wa Pakistani Nawaz Sharif horseedmedia.net

Waziri Mkuu wa Pakistan Nawaz Sharif amejiapiza kuendelea kutoa ushirikiano wa karibu kwa mataifa ya Magharibi lengo likiwa ni kuhakikisha nchi hiyo inapiga hatua za haraka kuelekea kwenye maendeleo sambamba na kuimarisha uchumi wake. 

Matangazo ya kibiashara

Kauli yake inakuja kipindi hiki viongozi wa Magharibi wakiendelea kumtumia salamu za pongezi kutokana na kufanikiwa kurejea tena madarakani kwa mara ya tatu mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu nchini humo Juma lililopita.

Uchaguzi Mkuu nchini Pakistan umepongezwa na waangalizi wakiwemo wale wa Umoja wa Ulaya EU ambao wamekiri licha ya uwepo wa dosari chache lakini umeendeshwa kwa misingi ya kidemokrasia.

Waziri Mkuu Nawaz Sharif anakabiliwa na kibarua kigumu cha kuhakikisha anaimarisha uhusiano na mataifa jirani ikiwemo India ambayo mara kadhaa wamejikuta wakiingia matatani wakigombea Jimbo la Kashmir.