Urusi

Urusi kumtimua mpelelezi wa Marekani nchini humo

Ryan Fogle jasusi wa marekani anayedaiwa kufanya kazi nchini Urusi
Ryan Fogle jasusi wa marekani anayedaiwa kufanya kazi nchini Urusi channelstv.com

Serikali ya Urusi imetangaza kumtimua mara moja afisa wa Shirika la Kijasusi la Marekani ambaye alikuwa anafanyakazi zake chini ya mwamvuli wa nchi hiyo huko Moscow akituhumiwa kufanya upelelezi.

Matangazo ya kibiashara

Jasusi huyo ametambulika kwa jina la Ryan Fogle ambaye alikamatwa katika Jiji la Moscow akiwa amevaa nywele za bandia ambazo zimekuwa zikivaliwa zaidi na wanawake sehemu mbalimbali.

Serikali ya Moscow imekuwa ikimhusisha jasusi huyo na kufanya shughuli za upelelezi ambazo zinaweza zikachangia kuibuka kwa machafuko baina ya nchi hizo mbili kwa kuwa haijulikani alikuwa anachunguza nini.

Taarifa kutoka Ubalozi wa Marekani huko Moscow zinaeleza Fogle alikuwa anafanya kazi kama moja ya watu wanaohusika na siasa lakini taarifa zinadai kuwa hakuwa akifanya kazi inayotajwa.

Wingu jeusi limeanza kutanda juu ya hatima ya uhusiano baina ya Marekani na Urusi katika siku za usoni kutokana na wengi kuhisi mataifa hayo yanaweza yakarejea kwenye vita baridi iliyokuwa inamalizwa.