Bangladeshi

11 wapoteza maisha, milioni moja wahamishwa kutokana na kimbunga Mahasen nchini Bangladesh

Kimbunga Mahasen
Kimbunga Mahasen livemint.com

Kimbunga aina ya Mahsen kimepiga nchini Bangladesh na kuua watu 11 na wengine wapatao milioni moja wakilazimika kuhamishwa kutoka katika makazi yao huku hofu ya madhara makubwa kutokea ikipungua baada ya kimbunga hicho kupungua kasi. 

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka nchini humo zimebaini miili 19 ya waislam wa madhehebu ya Rohingya kutoka nchi jirani ya Myanmar, ambao walipotea tangu kuzama kwa boti yao siku ya Jumatatu wakati wakikimbia kimbunga nchini mwao.

Mkuu wa polisi Mohammad Azad amesema kuwa miili hiyo iliyopatikana ni pamoja na 12 ya watoto, sita ya wanawake ambayo imepatikana kwenye ufukwe karibu na mpaka wa Myanmar na inadhaniwa kuwa miili hiyo ni ya waumini wa Kiislamu wa Rohingya.

Mamlaka zimepata ahueni baada ya kimbunga hicho Mahasen kilichokuwa na kasi kilomita 100 kwa saa kupungua kasi baada ya kupiga ufukweni na kusababisha maporomoko ya udongo.