Afghanistani

Rais wa Marekani Barrack Obama kuharakisha kuondoa Vikosi vya Marekani nchini Afghanistani

Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai
Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai REUTERS/Massoud Hossaini/Pool

Marekani inampango wa kuharakisha kuondoa vikosi vyake nchini Afghanistani kutaokana na hali ya mvutano uliopo kati yake na Rais wa Afghanistani, Hamid Karzai.

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Marekani, Barrack Obama anatarajia kumaliza kabisa operesheni za kijeshi nchini Afghannistani mwishoni mwa mwaka 2014 na Serikali yake imekuwa ikijadiliana na Serikali ya Kabul juu ya kuacha sehemu ya Jeshi la Marekani nchini humo.
 

Hakuna maamuzi yeyote yaliyofikiwa juu ya kuondolewa kwa Majeshi ya Marekani na idadi ya Wanajeshi watakaobaki, Maafisa wameeleza lakini wamesema lengo ni kuhakikisha amani ya kudumu inapatikana nchini humo.
 

Lakini Uhusiano kati ya Karzai na Obama umekuwa ukufifia hasa ni baada ya jitihada za Marekani kutaka kuanza kufanya mazungumzo ya amani na Wanamgambo wa Taliban nchini Qatar.
 

Karzai amepinga mazungumzo hayo, na kuishutumu Marekani kuwa inajaribu kufanya mazungumzo na Taliban na wanaowaunga mkono nchini Pakistani.
 

Hivi sasa, nusu ya Wanajeshi 68,000 wa Marekani nchini Afghanistani wanatarajiwa kuondoka nchini humo mwezi Februari na Jeshi, huku jeshi la Afghanistani limeendelea kuchukua jukumu la kulinda usalama nchini humo.